Uhalisia

演唱:Dicazzi
One and two, ile sana tuuu
Ama do or die ama die or do
Sivunjiki mkono sivunjiki guu
Utajipa tabu mi kiziwi sisikii la mkuu
Dunia ni nyumba Mbingu ndo paa la bluu
Siamini ndumba Mungu ndo Mganga Mkuu
Wino wakikubwa ka naiandika Juzuu
Verse iko timeless itaja skizwa na vitukuu
Chakula cha skio cha ajabu shida views
Wanaoimba wamekua wengi wanaoskiliza few
Chamuhimu nikuwapiga goli nyingi ka Ronaldo
Na kila ushangilio wa nikishinda SIIUUU
Okay, Money is the power
Utofauti mate na maji rangi sawa
Kujua unajua sio mpaka wakupe flowers
Ndo mana Mungu aliumba Malaika haitaji chawa
Luga gongana mandishi ya kizawa
mfano
Kuna sisi kuna wale kuna hawa
Kuna nyoka kuna Adam kuna hawa
Kuna seconds kuna minutes kuna hours
Who is next who is next
Wanapenda tabiri who is more who is less
Na Game ya skuiz hakuna who is wack who is best
Hustle zako movement ndo zita move net
Kimzunguko wa dunia nipo future
Shida wengi wenu mnawaza sasa
Misuko suko ya maisha imenifanya bado sija suka
Sana sana nawish kufuga rasta
Mshtuko nilipogundua utamu wa nachokitafuta utapungua sana siku nkipata
Na hii nikuacha legacy mmmhmm
kabla sijakufa
Namuomba Mungu kwa hamasa
Nshinde church nlale kanisani
Aimeen
Nipige salaa nimpuuzie shetani
Aimen
Iwe kwa muhamad Yesu Msalabani Aimen
Cha muimu kwamba dini isiishinde imani
Tunafanya mengi ya upumbavu na machache ya msingi
Tunatafuta pesa kidogo kuinjoi kwa wingi
Wanaotafuta pesa nyingi wanainjoi kidogo
Hizi harakati za madenge ama harakati za pimbi
Mtaani kugumu masela tushakata ringi
Tunaanza jitafta ukubwani sa tutapata lini
Uko unasoma uje ku graduate na miaka 20
Utafute kazi experience miaka 10 ishakua 30
Watoto wanamisaada
Wamama wanamisaada
Walemavu wana misaada
Watu wa upinde wana misaada
Achana na hao wadada wanaosaidiwa na wababa
Ujinga ni kwamba vijana tumeachwa tuwe vijana

你可能喜欢